Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir amtaja Nabi Bao bora CAF

Mudathir X Nabi Mudathir amtaja Nabi Bao bora CAF

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo kutoka Visiwani Zanzibar na klabu ya Young Africans Mudathir Yahya Abbas amefichua siri ya bao lake alilofunga dhidi ya TP Mazembe ambalo limeibuka Bao Bora la Kombe la Shirikisho Afrika Hatua ya Makundi kwa kusema Kocha Nasreddine Nabi alihusika.

Mudathir amesema, siri ya bao hilo ilitokana na maelekezo ya Kocha Nabi ambapo alimwambia siku hiyo kuwa ahakikishe anacheza nyuma ya washambuliaji wake ili yakitokea makosa afunge.

“Namshukuru Mungu kwa bao hilo ambalo naweza kusema nilifunga kwa msaada mkubwa wa makocha ambapo waliniambia siku hiyo nihakikishe nacheza nyuma ya washambuliaji jambo ambalo nilifanya hivyo na kujikuta nafanikiwa kupata nafasi ya kufunga,” amesema Mudathir.

Bao la Mudathir Yahya dhidi ya TP Mazembe limepigiwa kura na mashabiki kupitia ukurasa wa Twitter wa CAF na kupata asilimia 70.5

Chanzo: www.tanzaniaweb.live