Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir alivyoamua kuzungumzia Kiwanjani

Yanga Azam Mudathiri Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imefanya sajili za wachezaji mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi 8 iliyopita wakiwemo wazawa na wale wa Kimataifa.

Wapo ambao sajili zao zilitikisa mioyo ya wapenda soka na wapo ambao walionekana wa kawaida na wala hawakuzungumzwa mahala popote.

Miongoni mwa wachezaji ambao walionekana usajili wao ni wa kawaida ni Kiungo Mzanzibar Mudathir Yahya.

Wakati zinatoka taarifa Avic kuwa sajili mpya za Yanga hasa katikati zinaacha watu midomo wazi, kuna mtu mmoja anaitwa Mudathir Yahya ambae hata hazungumzwi sasa hivi lakini ndie kiungo pekee baada ya Pacome Zouzoua ambaye anaweza kucheza nafasi 3 tofauti (6,8,10) tena katika majukumu matatu tofauti, kiungo mkabaji, kingo wa sanduku kwa sanduku na mshambuliaji kivuli.

Tangu kutua kwa mudathir katika dirisha dogo la msimu uliopita amejihakikishia namba kikosi cha kwanza kuanzia kwa Kocha Nabi mpaka Muargentina Miguel Gamondi.

Wakati wengine wakizungumzwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Mudathir ameamua kuzungumza Kiwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: