Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir: Watu hawajui ninacheza namba ngapi uwanjani

Mudathir Yahya Simuu Mudathir Yahya.

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga SC, Mudathir Yahya amesema kuwa watu wengi hawaelewi uwanjani anacheza nafasi gani akiwa uwanjani kwani amekuwa akiwavuruga wapinzani na kupata nafasi ya kufunga mara kwa mara.

Mudathir amesema hayo akiwa na furaha baada ya kuandika rekodi nyingine akiiongoza timu yake kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga CR Belouizdad mabao 4-0 huku yeye akifunga bao la kwanza.

“Ngoja niwaibie watu siri, hawaelewi mimi nachezaje? Mimi sichezi kama kiungo sasa hivi, ninacheza kama winga asiyeeleweka. Kwa sababu timu yetu ina mawinga wanaocheza midfield, hawakai sehemu yao kwa hiyo mimi ninatakiwa nitoke niende nje niingie ndani.

“Tumeshamaliza mchezo, huko Misri kwa Al Ahly tunakwenda kutembea tu. Mwarabu nampa pole sana, alitukanda tatu kwake tukaonekana wapwelapwela, hatujui kumbe zamu yetu ilikuwa leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live