Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mudathir: Natamani kucheza timu moja na Fei Toto

Fei Toto, Mudathir Mudathir: Natamani kucheza timu moja na Fei Toto

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Mudathir yahya Abbas amesema kuwa alitamani kucheza na feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' kwenye klabu moja lakini bahati mbaya walipishana wakati wa usajili.

Mudtahir ambaye aliwahi kusema kuwa anatamani kucheza na Fei kwa sababu hajawahi kucheza naye licha ya kwamba wote wanatoka Visiwani Zanzibar.

“Ingekuwa vizuri zaidi kwa sasa tungekutana kwa sababu sote ni wa nyumbani. Kiufupi Ligi inamalizika, tunakwenda kukutana Zanzibar Heros, mtaona ushirikiano wetu,” amesema Mudathir.

Itakumbukwa kuwa, wakati Mudathir anatoka Azam FC anakwenda Yanga, Fei Toto yeye aliondoka Yanga na kwenda Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live