Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muda wowote Azam kumtambulisha Mcolombia

Navarooo 8 WA0000 Muda wowote Azam kumtambulisha Mcolombia

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda wowote kuanzia sasa, Azam FC inamtangaza straika wao mpya, Franklin Navarro raia wa Columbia.

Mwanaspoti limeandika ujio wa mchezaji huyo aliyeingia nchini jana jioni, huku viongozi wa timu hiyo wakisema utaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, lakini pia unaweza ukawa ndio mwisho wa Idris Mbombo, anasemekana anaweza akakatwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, inaelezwa ni mtalamu wa kucheka na nyavu na ana kasi ya kukimbia.

Chanzo cha taarifa kutoka ndani ya timu hiyo kimesema; "Muda wowote kuanzia sasa anasaini, tunatarajia uongezeko la mabao, pia amesajiliwa kipa mpya anaitwa Mohamed Mustafa anayeichezea timu ya taifa ya Sudan,"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live