Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muda wa usajili kutajirisha wajanja wajanja

Willy Onana X Gift Fred Muda wa usajili kutajirisha wajanja wajanja

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kalenda yangu inanionyesha kuwa leo ni Desemba 8 na zimebaki siku nane tu ili dirisha dogo la usajili kwa timu za Ligi Kuu ya NBC, Ligi ya Championship na ile ya wanawake kufunguliwa.

Hapa timu zinapata fursa ya kuimarisha vikosi vyao kulingana na mahitaji ambayo kila moja imeyapata kulingana na tathmini ya mabenchi ya ufundi kwa michezo ambayo imeshachezwa ya mwanzoni mwa msimu.

Huu ndio muda wa mavuno kwa wachezaji hasa wale walioonyesha viwango vizuri kwenye timu tofauti ambapo wanaweza kupata malisho ya kijani zaidi kwingine au ndani ya timu zao kwa kuongezwa mikataba mipya.

Kipindi kama hiki kinahitaji umakini mkubwa kwa timu na hata wachezaji kwani vinginevyo wanaweza kuingia mkenge ambao baadaye huacha majuto au kusababisha hasara ya kifedha hata kimatokeo.

Umakini mkubwa unahitajika dhidi ya kundi fulani la wajanja ambao husimama kama watu wa kati katika usajili baina ya klabu na wachezaji kwa lengo la kupiga cha juu kwani hao ndio mara nyingi huwa chanzo cha sajili nyingi kutozaa matunda.

Hawa hutumia mbinu mbalimbali kupandisha chati wachezaji wasio na uwezo na kuzishawishi timu ziwasajili ili tu wapate fungu na wale wanaostahili hupigwa vita kwa vile tu hawawezi kunufaika nao ikiwa watajiunga na timu.

Wanaweza kupandisha thamani kwa mchezaji zaidi ya ile halisi ili tu wapate fungu la ziada kupitia usajili huo jambo linaloweza kufanya usajili ukwame na kuharibu kesho za wachezaji lakini pia kuzifanya timu zitumie kiasi kikubwa zaidi cha fedha kwa wachezaji ambao hazikupaswa kutumia kiasi hicho.

Mara nyingi hawa jamaa huwatumia makocha wa timu kupendekeza wachezaji wao au hata baadhi ya viongozi ambao huwakatia fungu la fedha ili kulainisha mambo.

Ni wakati wa kuwa makini huu, sivyo watu watauziwa mbuzi kwenye gunia.

Chanzo: Mwanaspoti