Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muargentina kumrithi Nabi Yanga?

Miguel Angel Gamondi Miguel Ángel Gamondi

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuondoka kocha Nabi, klabu ya Yanga imeanza mchakato wa kumsaka Kocha mpya atakaekuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Raia huyo wa Tunisia anaetajwa kujiunga na Kaizer Chiefs.

Taarifa zinadai kuwa Yanga imeanza mazungumzo ya mkataba na Miguel Ángel Gamondi. Miguel ni kocha kutoka Argentina anayekinoa kikosi cha Ittihad Tanger (Morocco).

Kocha huyo ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika kwani kashawahi kuwa kocha mkuu katika klabu za Mamelodi Sundowns, USM Alger, Wydad Casablanca, Platinum Stars na CR Belouzidad.

Gamondi pia kashawahi kuwa kocha msaidizi timu ya taifa ya Burkina Faso na Esperance Sportive de Tunis.

Mwananchi una lipi la kusema hapo/ Tuachie "Comment" yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: