Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muargentina amuita Djuma kuivaa Stars

Djuma Djuma Shaban

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Mkuu wa DR Congo Hector Cuper amemjumuisha beki wa Yanga Djuma Shaban katika kikosi cha mastaa 26 wanaokuja kupambana na Taifa Stars katika mchezo wa hatua ya makundi kuwania kushiriki Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Stars ambao ndio vinara wa kundi J wakiwa na pointi 7 wanawakaribisha Congo wanaoshika nafasi ya tatu katika kundi hilo wenye pointi 5, mchezo utakaopigwa Oktoba 11 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Baada ya mchezo huo Congo maarufu kama Leopards watarudi nyumbani kuwakaribisha Benin huku Stars nao wakienda ugenini kuwafuata Madagascar katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Katika kikosi hicho Cuper amewaita makipa Kiassumba Joel (Sans Club), Mpasi Lionel (Rodez, Ufaransa), na Lomboto Herve (DC Motema Pembe ya Congo).

Wamo mabeki 9 ambao ni Djuma (Yanga), Idumba Fasika (Cape town City, Afrika Kusini), Marcel Tisserand (Fernabahce, Uturuki),Christian Luyindama (Galatasaray, Uturuki), Chancel Mbemba(Porto,Ureno),Mukoko Amale (El Jadida,Morocco),Glody Ngonda(Roga,Latvia), Fabrice N'sakala (Besiktas,Uturuki) na Arthur Masuaku(Westham United,Uingereza).

Viungo wamo Samuel Bastien (Standard Liege,Ubelgiji),Edo Kayembe(K.A.S. Eupen,Ubelgiji),Fabrice Ngoma (Raja,Morocco),Samuel Moutussamy(Nantes,Ufaransa),Gael Kakuta(Lens,Ufaransa),Neeskens Kebano (Fulham,Uingereza),Chadrac Akolo(Amiens,Ufaransa).

Washambuliaji wamo Cedric Bakambu (Beijing,China),Joel Ngandu( FC Viktoria Plzeƈ,Czech),Ben Malango(Sharjah,UAU),Dieumerci Mbokani(Kuwait FC,Kuweit),Jackson Muleka(Standard de Liege,Ubelgiji),Shadrac Muzungu (RS Berkane,Morocco) na Yannick Bolasie (Rizerspor,Uturuki).

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz