Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muamala wa Prince Dube kwenda Azam wakwama njiani

Dube Na Azam Kuanza Kupambana Kuanzia Kesho.jpeg Muamala wa Prince Dube kwenda Azam wakwama njiani

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa zilizo thibitika ni kwamba Prince Dube amelipa kiasi cha dola za Marekani 200,000 (takribani Tsh milioni 522) kwenda kwa Azam FC ili kuwa huru.

Dube alifanya malipo hayo siku ya ijumaa jioni na kutuma vithibitisho vya malipo kwa uongozi wa Azam, uongozi wa Azam unakiri kupokea vithibitisho vya malipo hayo lakini mpaka sasa bado pesa hiyo haijafika kwenye akaunti ya Azam.

Dube alipaswa kulipa kiasi cha $300,000 (Tsh 783) kwa Azam ili kuwa huru, baada ya majidiliano ya pande zote mbili wakafikia makubaliano ya $200,000 na ndio yaliyo fanyika. Kwa mantiki hiyo Dube amelipa pesa yote inayo takiwa kulipwa.

Kinacho subiriwa sasa ni kiasi hiko cha pesa kuakisi kwenye akaunti ya Azam fc na kisha klabu kutoa tamko rasmi ya kumaliziana/kuachana na mchezaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live