Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtunisia awapa dawa Yanga

Kikosi Cha Yanga Dhidi Ya Geita Mtunisia awapa dawa Yanga

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nahodha wa Yanga,Bakari Mwamnyeto amesema Aprili ni mwezi dume kwao kutokana na mitego ya mechi wanazokabiliana nazo, lakini uwepo wa Helmy Gueldich raia wa Tunisia amewalainisha mambo.

Ndani ya mwezi huu, wamekutana na Geita Gold mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kushinda wametinga nusu fainali ambapo watakutana na Singida Big Stars.

Ukiachana na hilo, mechi za Ligi Kuu wanakutana tena na Kagera Sugar leo, mchezo wanaohitaji kushinda ili kuendelea kuusogelea ubingwa maana wanahitaji pointi 11 ili ifikishe pointi 76 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba hata ikishinda michezo yake sita iliyosalia, hata hivyo bado wana mchezo wa hatua ya robo fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United.

"Mwezi huu tumekumbana na mechi ngumu kwenye ASFC tulihitaji kushinda ili kwenda nusu fainali, kwenye Ligi angalau tushinde nne kati ya sita ili tujihakikishie ubingwa lakini pia kuna robo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

"Tunakutana na timu ngumu mfano Kagera Sugar ina wachezaji wazuri, mechi inayofuata ni Simba watani wetu wa jadi, hivyo tutatakiwa kupambana zaidi kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,"anasema staa huyo wa zamani wa Coastal Union.

Alisema kinachowasaidia kushinda ni uwepo wa makocha wazuri ambao wanawafanya wawe na utimamu wa mwili na akili; "Kocha Nabi ni mtaalamu wa kujenga akili za wachezaji kuamini kufanya mambo makubwa. Pia yupo kocha wa viungo ambaye anahakikisha muda wote tunakuwa fiti, hiyo pia kocha inampa nafasi ya kutumia wachezaji wote waliopo hivyo ni kazi kwetu kumuonyesha kwamba tunastahili kuaminiwa."

Chanzo: Mwanaspoti