Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Tresor Mputu asaini Ufaransa

Obed Mputu Obed Mputu

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Obed Mputu (17) mtoto wa Gwiji wa TP Mazembe,Trésor Mputu ambaye aliitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa ajili ya kuitumikia Paris FC ya Ligi daraja la pili Ufaransa.

Mwaka wa 2009 Tresor Mputu aliisaidia klabu ya TP Mazembe kubeba taji la Ligi ya Mabingwa wa soka Afrika baada ya miaka 41.

Mputu alijipatia umaarufu mwaka 2007, wakati alipomaliza michuano ya ligi ya vilabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho akiwa mfungaji bora.

Mazembe walishindwa kufikia hatua ya makundi mwaka huo, lakini walikaribia nusu fainali 2008.

Wakati Mputu mwenye umri wa miaka 23, alipoendelea kukomaa kama mchezaji, alipewa unahodha wa TP Mazembe yenye makazi yake Lubumbashi na kufanikiwa kubeba kikombe hicho mwaka 2009.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live