Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Ronaldo kama mshua wake tu

Critiano Jr Ms Cristiano Junior

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Cristiano Ronaldo akiendelea kuchana nyavu katika mechi zake mbili za mwisho huko Saudi Arabia, mtoto wake, Cristiano Junior pia kinathibitisha kuwa mwanasoka hodari chipukizi.

Kinda huyo ambaye amewahi kunolewa na akademi za Manchester United, Real Madrid na Juventus kwa sasa yuko Saudia pamoja na baba yake.

Katika video inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Cristiano Jr alirekodiwa akifunga bao la ufundi.

Mchezaji huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 12, alitikisa wavu kwa shuti kali kupitia mguu wa kushoto huku akitulia katika mazingira yake mapya.

Mwanawe Cristiano Ronaldo ataendelea na taaluma yake ya soka nchini Saudi Arabia akinolewa na Mahd Academy baada ya baba yake kuhamia Al Nassr hivi majuzi.

Fowadi huyo wa zamani wa Manchester United kwa sasa ndiye mwanasoka anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani baada ya kujiunga na Al Nassr.

Mashabiki wake kote ulimwenguni sasa watapata fursa ya kutazama mchezo wake kwenye televisheni.

Bao la Ronaldo dhidi ya Al-Fateh lilifungua lango lake la kupachika mabao huku mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid akipachika mabao manne wiki iliyopita, Daily Mail inaripoti.

Mabao yake manne yaliisaidia Al-Nassr kupaa kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Saudia na watatarajia kuongeza pengo kubwa siku ya Ijumaa watakapocheza na Al-Taawon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live