Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Rivaldo asajiliwa Ureno

Rivaldo Joao.jpeg Mtoto wa Rivaldo asajiliwa Ureno

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa Mkongwe wa soka nchini Brazil Rivaldo, Joao Vitor amesaini mkataba na Klabu ya Vizela ya nchini Ureno.

Joao Vitor (17) ambaye ni kiungo ameondoka Atletico Guara FC ya Brazil ambapo ni nyumbani kwao na kujiunga na Ligi ya Primiera.

Rais wa klabu ya Vizela Joaquim Ribeiro amesisitiza kuwa ujio wa kiungo huyo umetokana na mapendekezo mazuri na kuwa jina la baba yake halikumfikisha hapo. "Hajaja sababu ya Rivaldo, amekuja sababu ana ubora wake, baba yake hajachangia lolote kwenye ujio wa Joao.

Rivaldo kama rafiki wa watu wa Vizela, kijana huyu tutamhakikishia usalama na mazingira mazuri ya kazi. Tunaamini hapo mbeleni atakuja kuwa ni mchezaji mkubwa wa kimataifa.

Rivaldo (50) ambaye kwa sasa anishi Orlando, Florida nchini Marekani alikuwa na historia ndefu katika soka ambapo amewahi kucheza Brazil, Hispania, Italia, Ugiriki, Uzbekistan na Angola. Aliwahi kuchaguliwa na FIFA kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 1999 akiwa Barcelona.

Mwaka 2002 alishinda Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Taifa ya Brazil. Amewahi kuchezea vilabu 13 vikiwemo vya nchini Brazil, Spain, Italy, Greece, Uzbekistan na Angola.

Watoto wake Joao na Rivaldinho, ambaye anakipiga Romanian katika Klabu ya Universitatea Craiova, wanafuata nyayo za baba yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live