Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Phil Foden alamba dili la mabilioni

Ronnie Foden Phil Foden Mtoto wa Phil Foden alamba dili la mabilioni

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari njema kutoka kwa Phil Foden, ambaye ni mchezaji wa Man City ni kwamba mtoto wake Ronnie Foden maarufu kama "El Wey" ameingia mkataba na kampuni ya Mitindo pamoja na kusimamia maisha na baadhi ya vipaji kutoka nchini Uingereza #PropelTalentgroup .

Ronnie atapokea kitita cha €10,000 ambazo ni sawa na Tsh milioni 34 kwa kila post atakayochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni 3.8.

Ronnie amekuwa maarufu mitandaoni baada kushiriki kwenye sherehe pamoja na baba yake baada ya Man City kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Inter Milan kwenye mchezo wa fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live