Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Kluvert afuata nyayo za baba yake

Shane Kluvert 16 Mtoto wa Kluvert afuata nyayo za baba yake

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa Mkongwe wa soka na Nyota wa zamani wa Ligi ya England, Patrick Kluivert, amesaini mkataba wake wa kwanza na Barcelona.

Shane (16), amefuata nyayo za Baba yake na kutia sahihi hiyo leo ambapo ataichezea klabu hiyo kwenye kundi la vijana wa chini ya miaka 18.

Kijana huyo ni mshambuliaji kama baba yake. Alipewa ubalozi na kampuni ya Nike akiwa na miaka 9.

Patrick ambaye ni shujaa wa Uholanzi alipewa heshima ya kipekee akiwa Nou Camp baada ya kuisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa LaLiga mwaka 1999.

Aliwahi pia kushinda katika Ligi ya Mabingwa akiwa na Ajax mwaka 1995, na kuwapeleka Uholanzi kwenye nafasi ya nne katika Kombe la Dunia mwaka 1998.

Kwenye miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, alijulikana kama mmoja wa washambuliaji bora Duniani.

Aliwahi pia kuichezea Newcastle United kwa msimu mmoja mwaka 2004/2005.

Hivi sasa Kluivert ni Meneja wa timu ya Uturuki Adana Demirspor ambayo ina nafasi ya tisa katika Super Lig.

Watoto wengine wa Kluivert nao ni wanasoka, Quincy (26) aliwahi kuichezea timu ya vijana ya Ajax, Justin (24) anaichezea Bournemouth na Ruben (22) anaichezea timu ya Dordecht nchini Uholanzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live