Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Beckham atua Brentford mazima

Bildschirmfoto 2023 01 07 Um 09 43 31 Mtoto wa Beckham atua Brentford

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Romeo Beckham, mtoto wa pili wa nyota wa zamani wa England David Beckham, amejiunga na Ligi ya England katika timu ya Brentford B kwa mkataba wa mwaka mmoja na uwezekano wa kuongezwa kwa mwaka mwingine.

Beckham (20) amejiunga na timu hiyo akitokea Inter Miami klabu ambayo baba yake ni mmoja wa wamiliki.

Mwezi January mwanasoka huyo alijiunga na Brentford kwa mkopo, chini ya uongozi wa kocha Neil MacFarlane .

”Tumemuongeza Romeo kwenye kikosi chetu mwezi January na amekuwa akifanya vizuri sana” alisema MacFarlane.

”Najisikia vizuri sana kwakweli, wamenipokea vizuri tangu siku ya kwanza, nimependa kuwepo hapa” alisema Romeo.

Brentford haichezi kwenye Ligi bali hucheza kwenye mashindano ya Kombe na pia huandaa mechi za kirafiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live