Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoko wa Ten Hag msimu wa 2024-25

Ten Hag Anajiandaa Kwa Fainali Ya Kombe La FA Bila Kujua Mustakabali Wake Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imeingia dirisha hili la usajili wa mastaa ikiwa na bajeti ya Pauni 50 milioni tu, hivyo jambo hilo linamfanya Kocha Erik ten Hag na mabosi wake kuwa na kazi kubwa ya kufanya ili kunasa wachezaji inaotaka waje kuongeza nguvu kwenye kikosi.

Ten Hag amebakizwa kwenye kikosi hicho cha Man United baada ya kufanyiwa tathmini kwa zaidi ya wiki mbili na bilionea Sir Jim Ratcliffe.

Ratcliffe na wakurugenzi wake walikutana na makocha kadhaa iliyotaka waje kumbadili Ten Hag kabla ya kuamua kubaki na Mdachi huyo.

Kitu ambacho hakipingwi ni Man United ni lazima ifanye usajili kabla ya dirisha halijafungwa Agosti 30. Itapaswa kuuza baadhi ya wachezaji wake, isipokuwa makinda Kobbie Mainoo, Alejandro Garnacho na Rasmus Hojlund, ambao hao hawaguswi.

Casemiro, Jadon Sancho na Mason Greenwood wao chochote kinaweza kutokea, watapigwa bei endapo kama italetwa ofa nzuri mezani. Man United inahitaji Pauni 40 milioni kwenye mauzo ya Greenwood na Sancho pia. Victor Lindelof, Christian Eriksen na Donny van de Beek, nao wapo kwenye kundi la wanaoweza kufunguliwa mlango wa kutokea, huku kila mmoja akiwa amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake.

Taarifa za hivi karibuni, Man United imefikia makubaliano binafsi na Jarrad Branthwaite na kilichobaki ni kukubaliana ada tu na Everton. Ikimnasa beki huyo anakwenda kucheza na Lisandro Martinez. Kwenye sehemu ya kiungo, Man United inasaka huduma za wakali Palhinha wa Fulham, Joao Neves wa Benfica, ambao wanaweza kugharimu Pauni 60 milioni na Pauni 84 milioni mtawalia.

Ipo kwenye mchakato pia wa kumsaka staa wa Monaco, Youssouf Fofana, ambaye wanachuana vikali na Arsenal katika kuwania saini yake. Imeelezwa kwamba Monaco ipo tayari kumuuza Fofana kwa Pauni 20 milioni tu.

Staa mwingine kwenye rada za Man United katika dirisha hili ni Mfaransa wa Crystal Palace, Michael Olise. Winga huyo mwenye umri wa miaka 22, amekuwa kwenye rada za timu nyingi, wakiwamo Chelsea na saini yake inaweza kupatikana kwa Pauni 60 milioni.

Wakati huo, Man United inaamini itabaki na kiungo na nahodha wao, Bruno Fernandes, ambaye amedaiwa kuwapo kwenye rada za klabu za Barcelona na Bayern Munich zinazohitaji huduma yake. Fernandes, atakayetimiza umri wa miaka 30, Septemba mwaka huu, anataka aongezwe mshahara kwenye mkataba wake mpya ili kuwa sawa kwenye daraja la malipo na mastaa Casemiro, Sancho na Marcus Rashford.

Kwenye fowadi, Man United inataka kumtafuta mchezaji wa kucheza na Hojlund na kwenye hilo wametegesha rada yao huko Wolves kwa mchezajiMatheus Cunha, ambaye pia anaweza kuwagharimu Pauni 60 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti