Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoko wa Simba kimataifa uko hivi...

Simbaaaa Sc Mtoko wa Simba kimataifa uko hivi...

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imepangwa kundi moja C na miamba ya Morocco, Raja Casablanca.

Katika droo hiyo ambayo imepangwa huko Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Cairo, Misri ilishuhudiwa Yanga ikiwa klabu ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kufahamika wapinzani wake watatu, TP Mazembe, US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya Mali ambao amepangwa nao kundi D.

Muda mchache baada ya kukamilika kwa droo hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo miongoni mwa waendeshaji 'wachezeshaji' alikuwepo nyota wa zamani wa timu ya taifa la Angola na klabu ya Al Ahly, Flavio Amado ilifuata ya Ligi ya Mabingwa na kushuhudiwa Simba ikipangwa kundi C na Raja Casablanca, Horoya AC na Vipers.

Simba ambao msimu uliopita walifika hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho, hii ni awamu yao ya 12 kushiriki michuano hiyo mikubwa zaidi Afrika ngazi ya klabu, msimu uliopita 2021–22 waliishia raundi ya pili ambapo walitolewa na Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla (3-3).

Raja Casablanca wametwaa mara tatu Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye miaka ya 1989, 1997 na 1999 kwa sasa wananjaa ya zaidi ya miaka 20 bila ya kombe hilo ambalo kwenye miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakiishia hatua ya robo, nusu na fainali.

Kwa upande wa Horoya AC yenye maskani yake Conakry, Guinea huu ni msimu wao wa 13 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mafanikio makubwa kwao ni kufika robo fainali ambapo ilikuwa kwenye miaka ya 2018 na 2019, uliopita waliishia makundi.

Vipers ni wawakilishi wa Uganda ambao Agosti mwaka huu walishuhudiwa nchini kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, ni miongoni mwa timu shindani ukanda huu.

Chanzo: Mwanaspoti