Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoko wa Pochettino utakuwa balaa kubwa United

Skysports Mauricio Pochettino 5523923 Mauricio Pochettino

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Manchester United inajiandaa kufanya mabadiliko makubwa kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kwa ajili ya kuunda kikosi cha kazi cha msimu ujao.

Kocha wa kipindi cha mpito, Ralf Rangnick anajiandaa kubadilishwa na kocha wa Paris Saint-Germain, Mauricio Pochettino kwenye benchi la ufundi la miamba hiyo ya Old Trafford.

Pochettino, 49, amewekwa kwenye mipango ya Man United ambayo kwa sasa haionekani inacheza staili gani ya soka lake na kinachoelezwa ni kwamba Muargentina huyo akitua tu Old Trafford, usajili wake wa kwanza atakaofanya ni kumnasa Harry Kane.

Ujio wa Kane bila ya shaka utamweka pembeni Cristiano Ronaldo kwenye kikosi kama atakubali kuendelea kubaki mahali hapo. Jadon Sancho kwa sasa tayari ameshajitengenezea nafasi kwenye wingi ya kushoto na bila ya shaka Pochettino ataendelea kumtumia atakapotua klabuni hapo.

Mpango wa Man United ni kumnasa staa wa Kibrazili, Antony, anayekipiga huko Ajax kuja kucheza wingi ya kulia. Winga huyo Mbrazili amefunga mabao 11 na kuasisti mara nane msimu huu na kuwavutia Man United.

Bruno Fernandes, atabaki kwenye majukumu ya kucheza kiungo ya kushambulia chini ya Pochettino, ikiwa ni wazi alihitaji saini yake wakati alipokuwa Spurs mwaka 2019, bila shaka atakuwa Namba 10 kwenye fomesheni pendwa na Muargentina huyo ya 4-2-3-1.

Nyuma ya fowadi hiyo iliyosheheni mastaa watupu, Pochettino atahitaji kuwa na safu ya kiungo itakayokuwa na wakali wapya.

Man United ipo kwenye mchakato wa kunasa saini ya staa wa West Ham, Declan Rice kwenye dirisha lijalo na huenda saini yake ikagharimu Pauni 100 milioni.

Kwenye dili hilo, Man United inaweza kuamua kuwa na pacha ya Rice na Kalvin Phillips, huku pia ikiwa kwenye mchakato wa kumnasa Amadou Haidara kutoka RB Leipzig kama watamkosa Phillips.

Man United ya msimu ujao kama itamchukua Pochettino bila ya shaka hatakuwa na shaka kwenye safu ya mabeki, ambapo Harry Maguire na Raphael Varane wataendelea kuwa pacha katikati, huku pembeni ni Aaron Wan-Bissaka na Luke Shaw na David de Gea atasimama golini kama kawaida.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz