Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoko wa Big Six dirisha la Januari 2024

Tdfdyd Mtoko wa Big Six dirisha la Januari 2024

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Dirisha la Januari la usajili wa mastaa limebakiza siku chache sana kufunguliwa na sasa kila timu ishafahamu ni wapi inahitaji kufanya maboresho ili kumaliza msimu kibabe.

Huko kwenye Ligi Kuu England, wale wababe wa Big Six kila timu ishafahamu ni wapi au ni nani wa-kumwongeza kwenye kikosi kwenye dirisha hilo la Januari ili kufanya vikosi vyao kuwa vya kibabe zaidi ndani ya uwanja.

Nusu ya kwanza ya msimu huu imeshachezwa, kila kocha sasa kwenye vikosi hivyo vya Big Six – Pep Guardiola wa Manchester City, Mikel Arteta wa Arsenal, Jurgen Klopp wa Liverpool, Erik ten Hag wa Manchester United, Mauricio Pochettino wa Chelsea na Ange Postecoglou wa Tottenham Hotspur kila mmoja ameshafahamu ni wapi pa kuongeza wakati dirisha la Januari litakapofunguliwa.

Katika dirisha hili la Januari, Makala haya yanahusu wachezaji ambao vigogo wa Big Six watakuwa wamejiweka pazuri Ligi Kuu England kama ikifanikiwa kunasa saini zao na kuwafanya waende kukipiga kwenye timu zao.

Arsenal - Dominic Solanke

Anakocheza sasa: Bournemouth

Ndoto za Arsenal za kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England zinahitaji kufunga mabao mengi zaidi sam-bamba na kuwa na safu bora ya ulinzi, ambayo kwa sasa imekuwa kwenye uimara mkubwa chini ya William Saliba na Gabriel, wakisaidiwa na kiungo wa ukabaji, Declan Rice. Kocha, Mikel Arteta anaon-ekana kumaliza tatizo kwenye eneo hilo na sasa nguvu yake anataka kuongeza mabao ya kufunga ili kikosi kiwe kwenye uwiano bora kabisa na nguvu ya kunyakua taji.

Gabriel Jesus ni mshambuliaji mzuri, lakini amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi yanayomfanya kocha Arteta ashindwe kuwa na uhakika wa huduma yake na hivyo mara kadhaa kulazimika kumtumia Eddie Nketiah.

Kutokana na hilo, straika Dominic Solanke amewekwa kwenye mipango ya miamba hiyo ya Emirates, hasa baada ya staa huyo kufanya vizuri sana huko Bournemouth. Arteta anaamini kwa kuwa na hudu-ma ya Solanke itafanya kikosi chake kiwe matata.

Liverpool - Joao Palhinha

Anakocheza sasa: Fulham

Liverpool imejipata baada ya kutengeneza kiungo mpya inayoundwa na Dominik Szoboszlai, Alexis Mac Allister, Wataru Endo na Ryan Gravenberch. Shughuli yao ni pevu. Wachezaji wote hao wane wamesajiliwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka huu kuna kuwabadili Jordan Henderson, James Milner, Fabinho, na Naby Keita. Katika orodha yote hiyo, Endo peke yake ndiye kiungo wa asili wa kukaba, aliyekuja kuziba pengo la Fabinho, lakini mkali huyo wa zamani wa Stuttgart amekuwa aki-tumika na Kocha Jurgen Klopp kwa mtindo wa kubadilishabadilishana.

Staili ya uchezaji ya miamba hiyo ya Anfield inahitaji wapambanaji kweli kweli kutokana na Klopp anavyotaka timu yake icheze. Uhitaji wao wa kutaka kutawala mchezo umemfanya Mac Allister awe anacheza chini sana, jambo ambalo linatoa nafasi kwa timu hiyo kwenda kumsajili Joao Palhinha kuja kucheza eneo hilo ili Mac Allister apande juu.

Man City - Florian Wirtz

Anakocheza sasa: Bayer Leverkusen

Vipi kuhusu Manchester City? Kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola kinaonekana kukamilika karibu kwenye kila eneo. Kiungo wao mshambuliaji, Kevin de Bruyne ana miaka 32 sasa na majeruhi ya-meanza kumsumbua, kitu ambacho miamba hiyo ya Etihad inapambana kuhakikisha inaleta mtu wa kuchukua nafasi yake mapema.

Wirtz amekuwa kwenye kiwango bora sana katika kikosi cha Bayer Leverkusen kinachonolewa na Xabi Alonso, hivyo Man City wanamtazama kama mtu ambaye anawafaa kuja kupiga mzigo huko Etihad.

Kikosi cha Alonso kinashindania ubingwa na Bayern Munich huko kwenye Bundesliga, huku ikiendelea kupambana pia kwenye michuano ya Ulaya, hivyo hawaonekani kama watakuwa tayari kuachana na Wirtz kwenye dirisha la Januai. Licha ya nguvu ya kifedha ya Man City, Leverkusen wanaweza kukomaa kwenye vita ya kumbakiza fundi huyo wa mpira wa Kijerumani kwenye timu yao walau hadi mwisho wa msimu.

Tottenham – Ivan Toney

Anakocheza sasa: Brentford

Kocha Ange Postecoglou hakupata fursa ya kumtumia straika Harry Kane kwenye mechi za Ligi Kuu England kama mshambuliaji wake kiongozi kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur. Wakati Richarlison akipambana na kuwa na viwango vya kutosha, lakini Mbrazili huyo ameshindwa kuwa mchezaji anayeweza kutumia kwa usahihi nafasi anazopata ili kufunga mabao kama ambavyo amekuwa akifanya straika Ivan Toney. Brennan Johnson alisajiliwa kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha lililopi-ta, lakini amekuwa akitumika kwenye winga ya kulia, hivyo Toney atakuwa na nafasi ya kuongoza mas-hambulizi ya Spurs.

Wasiwasi uliopo ni kama Toney atarejea uwanjani akiwa kwenye makali yale yale baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi minane.

Alifunga mabao 20 kwenye ligi msimu 2022/23 akiwa na Brentford, hivyo Spurs wanamtaka aje kucheza na Heung-min Son katika kuifanya safu ya ushambuliaji yao kuwa moto.

Man United - Donyell Malen

Anakocheza sasa: Borussia Dortmund

Mara kadhaa huko nyuma zilishuhudia uhamisho wa mchezaji kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United huwa hauna matunda mazuri, hilo likithibitishwa hivi sasa kupitia Jadon Sancho, anayewekwa tu kando na Kocha Erik ten Hag huko Old Trafford.

Winga huyo wa England, Sancho anaweza kurudi tena Dortmund, katika dili ambalo linaweza kumfanya Donyell Malen kutimkia zake Ligi Kuu England kwenda kuvaa uzi wa Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford.

Donyell Malen ni winga na ni Mdachi, hivyo anaweza kukubali kuja kucheza chini ya Mdachi mwenzake, Ten Hag. Malen anaweza kucheza pembeni au katikati kama ambavyo amekuwa akifanya Sancho. Man United inafahamu tofauti ya winga wao Antony na Malen, hivyo akija Old Trafford utakuwa usajili am-bao utaongeza nguvu kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao mara 20 wa England.

Chelsea – Mike Maignan

Anakocheza sasa: AC Milan

Kipa Robert Sanchez alisajiliwa kutoka Brighton mwanzoni mwa msimu kuna kumbadili Kepa Arriza-balaga – ambaye aliachana na Chelsea kutimkia zake Real Madrid kwa mkopo, lakini kipa huyo Mhis-paniola mambo yake si matamu sana Stamford Bridge.

Kutokana na hilo, Mike Maignan sasa ameibukia kama kipa anayesakwa kwa nguvu zote ili aje kuokoa jahazi kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge. Kwa kuwa Chelsea tajiri wao si bahiri wa kutua pesa, kuna uwezekano mkubwa akazama mfukoni ili kwenda kunasa saini ya kipa Mfarana, Maignan endapo kama Sanchez ataendelea kuboronga.

Shida inakuja sehemu moja, AC Milan bado ipo kwenye michuano ya Ulaya – ikikabiliwa na mikikimikiki ya Europa League – hivyo wanaweza kuleta shida kwenye kumpiga bei kipa wao.

Hata hivyo, wanasema pesa ni kilainishi, AC Milan wanaweza kubadili mawazo yao na kumpiga bei Maignan wakiwekewa mzigo wa maana mezani na The Blues.

Chanzo: Mwanaspoti