Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtihani wa kwanza wa Rangnick upo mikononi mwa Crystal Palace

Rangnick Vibali Kocha Mpya wa Man United, Ralf Rangnick

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutangazwa rasmi kama kocha wa muda wa Manchester United, sasa ni rasmi, Ralf Rangnick ataanza kazi ya kuiongoza United dhidi ya Crystal Palace.

Rangnick ametua United kwa mkataba wa kuiongoza timu hiyo kwa miezi 6 kama kocha wa mpito kisha, ataendelea kufanya kazi na United kama mshauri kwa miaka miwili.

Kutangazwa kwa Ralf Rangnick ilikuwa ni hatua ya kwanza, kuanza kazi rasmi ni hatua ya pili. Kufuatia taratibu za kufanya kazi nchini Uingereza, Rangnick alikuwa akisubiri kibali cha kumuwezesha kuanza kazi yake pale Old Trafford.

Mvumilivu hula mbivu, Rangnick amepatiwa kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza na sasa ni rasmi, mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Crystal Palace jumapili hii ndani ya Old Trafford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live