Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtihani wa kwanza kwa Kocha Pablo

Pablo Pic Simba itavaana na Ruvu Shooting

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema anatarajia mchezo mzuri dhidi ya Ruvu Shooting Ijumaa huku matarajio yake yakiwa ni kuanza kwa ushindi.

Pablo amesema amewaona wapinzani wake dhidi ya Yanga ameshuhudia mchezo wenye kasi na nguvu hivyo anatarajia kuona mechi bora na ya ushindani.

“Ni mechi yangu ya kwanza natamani kuona nikipata matokeo ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuendeleza ushindani,” amesema.

Pablo amesema maandalizi kwa upande wa wachezaji walikuwa mazuri kilichobaki ni utekelezaji na anatarajia nyota wake kuto kumuanguza kwa kile alichokifanya wakati wa maandalizi.

Amesema wachezaji waliopo wanatosha kuamua matokeo Ijumaa dhidi ya Ruvu Shooting huku akisisitiza kuwa anawaheshimu wapinzani wake na anaamini watatoa changamoto kwa timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live