Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtihani mzito kwa Yanga mchezo wa Kimataifa

Yanga Janja Janja.jpeg Mtihani mzito kwa Yanga mchezo wa Kimataifa

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi ya CAF Champions League Nov 24 mwaka 2023, Ugenini nchini Algeria.

Wakati huohuo timu za taifa zipo kwenye mashindano ya kufuzu kombe la Dunia na asilimia kubwa ya wachezaji wa Yanga wanaocheza kikosi cha kwanza wapo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa Kufuzu kwa Kombe la Dunia.

1.Mudathir Yahya- TZ

2.Metacha Mnata- TZ

3.Aboutwaleeb Mshery- TZ

4.Bakar Mwamnyeto- TZ

5.Nickson Kibabage- TZ

6.Dickson Job- TZ

7.Ibrahim Bacca- TZ

8.Clement Mzize- TZ

9.Khalid Aucho- UGANDA

10.Stephane Aziz Ki- B/FASO

11.Djigui Diarra - Mali

Tanzania Nov 18, 2023 itacheza ugenini nchini Morocco dhidi ya Niger na Nov 21, 2023 itacheza jijini Dar es Salaam dhidi ya Morocco.

Kikosi cha Yanga SC kinatarajia kuondoka kuelekea nchini Algeria Nov 22, 2023 halafu Nov24, 2023 itacheza dhidi ya CR Belouizdad.

Kalenda ya FIFA kuanzia November 15, 2023 hadi November 22,2023 kwa maana hiyo Kuna baadhi ya wachezaji ambao watakuwa mataifa mengine huenda wakaungana na timu moja kwa moja nchini Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: