Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa yathibitisha kumpokea Katwila

Katwila Mtibwa yathibitisha kumpokea Katwila

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mtibwa Sugar imethibitisha kuwa aliyewahi kuwa Kocha wao mkuu, Zubeir Katwila ni miongoni mwa makocha wazawa waliotuma CV zao kutaka kazi kwenye klabu hiyo na bado mazungumzo yanaendelea huenda akapewa kazi ya kukinoa kikosi hicho.

Hayo yamesemwa na msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru wakati akizungumza na Azam Tv mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Mtibwa dhidi ya Kagera Sugar ambapo, Wanamanungu wameambulia kipigo cha bao 2-0 wakiwa nyumbani.

Ikumbukwe kuwa Mtibwa kwa sasa hawana kocha baada ya kumtimua aliyekuwa Kocha wao, Habib Kondo kufuatia matokeo mabaya huku Zubeir Katwila naye akipigwa chini na Ihefu Fc ya mkoani Mbeya hivi karibuni.

"Ni kweli kwa sasa hatuna kocha mkuu lakini mchakato unafanyika haraka iwezekanavyo tuweze kupata kocha mwingine kabla ya mchezo ujao.

"Tumepokea CV za makocha watano wazawa na mchakato wa kuchambua CV zao unaendelea. Miongoni mwa makocha hao, ni Zubeir Katwila, kwa hiyo ni kazi kweli kweli kuchambua na kupata kocha tunayemtaka lakini niwahakikishie, hivi karibuni tutatangaza kocha mpya," amesema Kifaru.

Ikumbukwe kuwa, tangu kuondoka kwa Katwila kwenye Klabu ya Mtibwa Sugar, timu hiyo haijawa na nyakati nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ambapo kwa msimu huu haijashinda hata mchezo mmoja kati ya michezo sita ambayo imecheza.

Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu 23/24.

❌ Mtibwa 2-4 Simba

❌ Prisons 3-2 Mtibwa

❌ Mtibwa 0-1 Singida

☻ Dodoma 1-1 Mtibwa

☻ Mtibwa 1-1 Coastal

❌ Mtibwa 0-2 Kagera

— Mechi 6, Ushindi 0

Makocha ambao wametimuliwa msimu huu.

Hans Van pluijm - Singida BS

Zuber Katwila - Ihefe Sc

Habib Kondo - Mtibwa Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live