Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa yatangaza vita mzunguko wa pili

8c9acdd79fe29fd3d48eef28b5fe2f18 Mtibwa yatangaza vita mzunguko wa pili

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikitarajiwa kuendelea mapema mwezi ujao, Mtibwa Sugar, imetangaza hali ya hatari kwa timu pinzani.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru alisema wamedhamiria kupambana katika michezo ya lala salama ili kufanikisha lengo walilojiwekea msimu huu wa 2020/21.

Kifaru alisema hawataki kurudia makosa yaliyojitokeza msimu uliopita ambapo hali yao ilikuwa mbaya hadi kufikia hatua ya kuwa sehemu ya timu ambazo zilitarajiwa kushuka daraja.

“Tumejipanga kweli kweli, hatutakuwa na huruma na timu yoyote tutakayocheza nayo katika mzunguko huu wa pili, hatutaki yatufike ya msimu uliopita ambapo ilikuwa chupuchupu kushuka daraja.”

“Tumejidhatiti kufanya vyema tukiwa na kocha wetu mpya Hitimana Thiery ambaye tayari ameambiwa na uongozi nini Mtibwa Sugar inahitaji katika kipindi hiki,” alisema Kifaru.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imecheza michezo 18, ikiwa na pointi 22 zilizotokana na ushindi katika michezo sita, huku ikipoteza michezo nane na kuambulia sare mara nne.

Chanzo: habarileo.co.tz