Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa yamsaini Banda kutoka Afrika ya Kusini

Abdi Banda Beki Abdi Banda

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya msimu uliopita chupu chupu kushuka daraja, Klabu ya Mtibwa Sugar kutoka kule Manungu Morogoro, safari hii haitaki mchezo.

Mtibwa imejitahidi kufanya usajili wa kiwango kikubwa sana ili kujiimarisha na katika kuthibitisha hilo wamemnasa Said Ndemla kwa mkopo kutoka Simba, kiungo George Chota na sasa imenasa saini ya beki Abdi banda.

Katika taarifa yake iliyotolewa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Mtibwa imesema;

"Tumefanikiwa kuinasa saini ya beki wa kati mwenye ufundi mkubwa Sana na hadhi ya nchi Abdi Banda. Tumemsajili Banda kutoka katika klabu Ts Galaxy inayoshiriki ligi kuu Afrika Kusini".

Alpotafutwa ili azungumzie tukio hilo Banda amesema;

“Ujue mimi nilikuwa Sauzi kama mwezi hivi, nilifanya nao mazoezi wiki tatu na baada ya hapo wakaniambia mwenye timu hayupo nimsubiri mpaka aje,” alisema Banda na kuongeza;

“Wakati nikiwa namsubiri huku ikienda wiki ya nne nikapata Uviko 19 nikawekwa tu ndani mpaka nikae sawa, nilipokuja kukaa sawa wakaniambia wanipe tena wiki mbili zingine kitu ambacho niliona kama hawana nia na mimi.”

Kwa takribani misimu miwili iliyopita hali ya Mtibwa katika sugar ndani ya Ligi kuu imekuwa na kiwango hafifu hali iliyowalazimu kucheza michezo ya mtoano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live