Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa waitandika Singida Big Stars

Singida Big Stars Apocalypto Mtibwa yaibuka na ushindi wa bao 1-0

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao pekee la Charles Ilanfya dakika ya 63 limetosha kuipatia pointi tatu Mtibwa Sugar dhidi ya Singida Big Stars mchezo uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro.

Timu hizo zilikuwa zikihitaji ushindi baada ya mechi zao za mwisho kufungwa kufuatia Mtibwa Sugar kuchapwa mabao 2-1 na KMC Oktoba 15 wakati Singida BS ilifungwa 1-0 na Azam Oktoba 3.

Katika michezo minane iliyocheza Mtibwa Sugar msimu huu imeshinda mitatu, sare tatu na kupoteza miwili ikishika nafasi ya tatu na pointi 12.

Kwa upande wa Singida BS imecheza michezo sita ikishinda miwili, sare mbili na kupoteza miwili ikiwa nafasi ya 10 na pointi nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live