Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa waapa kutonesha kidonda Msimbazi

Farouk Shikhalo Mtibwa Simba wataikaribisha Mtibwa katika dimba la Mkapa leo Jumapili

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Mtibwa Sugar, Farouk Shikhalo amesema kiwango kizuri kinachoonyeshwa na timu yake kinawapa nguvu ya kuifunga Simba pale timu hizo zitakapokutana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa leo.

Timu hizo zinakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku Mtibwa Sugar ikiwa na matokeo mazuri ya kuibuka na ushindi baada ya kuzifunga 1-0 Singida Big Stars na Dodoma Jiji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Shikhalo alisema wana matumaini makubwa ya kuvunja uteja kwa Simba ingawa haitokuwa mchezo mwepesi kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Kikubwa ambacho tumekuwa tukihimizana sisi wenyewe wachezaji ni kuongeza juhudi kwenye kila mchezo, ligi ni ngumu na kupata matokeo chanya ugenini inabidi kupambana sana,” alisema.

Kiungo wa kikosi hicho, James Kotei ambaye amewahi kuichezea Simba alisema ili kuonyesha wako vizuri msimu huu watahakikisha wanatumia mchezo huo kuwaadhibu wapinzani wao.

Mechi hiyo haitarajiwi kuwa rahisi kwa Mtibwa kwani wanakutana na Simba ambayo mara ya mwisho walipokutana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 23 mwaka huu walifungwa 2-0.

Mtibwa mara ya mwisho kuifunga Simba ilikuwa 1-0, Februari 24, 2013.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live