Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa waapa kumtungua Mnyama leo

Thobias Kifaru Sokalabongo Mtibwa waapa kumtungua Mnyama leo

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtibwa Sugar wametamba kuwa, kikosi chao kipo sawa na maandalizi yote ya mchezo wao wa leo dhidi ya Simba SC, na hakuna wanachokihitaji zaidi ya ushindi.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru amesema msimu uliopita walifahamu matatizo yao, wamerekebisha kikosi hivyo wanaamini msimu huu wanakwenda kufanya vizuri.

"Tulikuwa na wachezaji wa kigeni kama watano tumeona hawana mchango wowote, tumeachana nao na sasa hivi kikosi kimesheni wazawa na tunaamini kwamba tunafanya vizuri," alisema Kifaru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live