Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa vs Kagera mechi ya kibabe leo

Sukari Pic Data Mtibwa vs Kagera mechi ya kibabe leo

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MECHI ya vuta nikuvute hii leo Aprili 17 itakayowakutanisha wakata miwa Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kila timu ikipambana kupata alama tatu za kuwaweka sehemu nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzana Bara.

Mtibwa ni mwenyeji wa ndugu zake wa Kagera mchezo utakaopigwa katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro huku timu hizo zikizidiana pointi mbili pekee.

Kagera anashika nafasi ya 14 akijitupa dimbani mara 25 akishinda michezo sita sare nane na kupoteza 11 huku Mtibwa akishika nafasi ya 15 akicheza mechi 24 na kushinda sita sare sita na kupoteza 12.

Mtibwa wao wanashuka  dimbani wakitoka katika maumivu makali ya kupigwa 5-0 na Simba huku Kagera Sugar akitoka sare ya bila kufungana na Mbeya City.

Thobias Kifaru ameiambia Mwanaspoti kuwa, mchezo wa leo utakuwa na ushindani baina ya pande zote mbili hivyo wao kama wenyeji watajitahidi kujipapatua kupata matokeo.

"Ni mechi ngumu na hasa ikizingatia sisi tuko nyumbani, na tumetoka kupata kilio kwenye mechi iliyopita, hali yetu ni mbaya sana ila tutapambana tu," amesema Kifaru.

Kifaru amesema, Kagera sio timu ya kubeza ni moja ya timu zenye ushindani mkubwa katika Ligi ya Tanzania hivyo wao wanaingia uwanjani na taadhari kubwa hii leo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz