Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa ni mtelezo tu, yaichapa Coastal Mkwakwani

Mtibwa Sugar 1 0 Kihimbwa akifunga goli la Mtibwa Mkwakwani

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya disemba 28, Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Bao pekee la Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Salum Kihimbwa kwa penalti dakika ya 27.

Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar imefikisha pointi 10 na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live