Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar yatoa tahadhari Ligi Kuu

Thobias Kifaru Ligalambwike Mtibwa Sugar yatoa tahadhari Ligi Kuu

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Mtibwa Sugar, umeweka wazi kuwa maandalizi ambayo wanafanya kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, yanapendeza, hivyo atakaye na aje kwani wapo tayari.

Timu hiyo inayotumia Uwanja wa Manungu uliopo Morogoro kwa mechi zake za nyumbani, ilianza kwa kupoteza dhidi ya Simba SC kwa mabao 2-4, kisha ikapata sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema kuwa, wanaendelea na maandalizi kwa mechi zinazofuata.

“Tupo tayari kwa ushindani msimu huu mpya na wapinzani wetu waje, hatuna mashaka kwa kuwa wachezaji wana uzoefu mkubwa katika kusaka matokeo ya ushindi.

“Kupoteza mchezo wa kwanza haimaanishi ligi imeisha, kazi bado inaendelea na tutafanya vizuri katika mechi zetu zijazo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Kifaru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live