Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar yatakata Manungu

Manungu Pic Mtibwa Sugar yaipa kichapo Ruvu Shooting

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Japokuwa ushindi wa mabao 3-1 iliyopata Mtibwa Sugar dhidi ya Ruvu Shooting, haujabadilisha chochote kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara zaidi  ya kujiimarisha.

Kabla ya mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Manungu, leo Jumatatu ya Juni 13, 2022,  Mtibwa Sugar ilikuwa nafasi ya 12 na pointi 28, kilichobadilika ni ongezeko la pointi (31) na mabao kutoka 26 hadi 29.

Wakati huo huo, Ruvu inaendelea kuwa na hali mbaya, imesalia nafasi ya 13, ikiwa na pointi 28 na imeongeza idadi ya mabao ya kufungwa kutoka 24 hadi 27 na ya kufunga kutoka 34 hadi 35.

Habari njema kwa Ruvu Shooting, Prisons iliopo nafasi ya 14 ikitokea ikaifunga KMC, haiwezi kupanda nafasi ya 13 kwani itafikisha pointi 28 sawa na za timu inayonolewa na Boniface Mkwasa (Ruvu).

Wafungaji wa mabao ya Mtibwa Sugar ni Brian Mayanja raia wa Uganda, dakika ya 56, 75 bao lingine alijifunga mchezaji wa Ruvu, aliyefahamika kwa jina la Kombo akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira dakika ya 41, bao la kufutia machozi la Ruvu limefungwa na Kassim.

Hiyo ni mechi ya tatu kwa Mtibwa Sugar kupata matokeo ya ushindi kwenye Uwanja wa Manungu.

Mechi nyingine ni dhidi ya  0-0 Simba (Januari, 22), Mtibwa Sugar 0-2 Yanga (Februari 23), Mtibwa Sugar 2-0 Geita Gold (Machi 13), Mtibwa Sugar 1-1 Kagera Sugar (Aprili 03), Mtibwa Sugar1-0 Mbeya City (Mei 7), Mtibwa Sugar 1-2 Azam (Mei 21) na Mtibwa Sugar  0-0 Coastal Union (Mei 15).

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz