Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar  yachapwa nyumbani

B5b3c2e258009e2f21338e13b016f2f4.png Mtibwa Sugar  yachapwa nyumbani

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MTIBWA Sugar imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Jamhuri mjini Morogoro baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa Sugar wameendelea kuwa wanyonge mbele ya Polisi Tanzania baada ya kupoteza michezo yote miwili waliyokutana na maafande hao, ambapo katika mzunguko wa kwanza walikubali kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Polisi walipata mabao yao kupitia kwa kiungo, Abdulaziz Makame katika dakika ya 33 na 40 lililofungwa na Tariq Seif, Mtibwa Sugar walipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Kelvin Kongwe dakika ya 51.

Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar iendelee kubaki katika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 28, wakati Polisi wakifikisha pointi 37 na kuwa sambamba na Tanzania Prisons wakiwa wameshuka uwanjani mara 28.

Chanzo: www.habarileo.co.tz