Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar ya 'ushindi' kusepa na pointi tatu leo?

Kagera Vs Mtibwa Mtibwa Sugar ya 'ushindi' kusepa na pointi tatu leo?

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mtibwa Sugar ni kama imepata kikosi chake cha ushindi baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kutobadili wachezaji katika mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu.

Baada ya kupata ushindi katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania, Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga ameendelea kukiamini kikosi chake ambapo leo ameingia na wachezaji waliompa ushindi kwenye michezo hiyo.

Mtibwa Sugar inavaana na Kagera Sugar muda mfupi ujao katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuanzia saa 8 mchana.

Kikosi hicho cha ushindi cha Mtibwa Sugar ni kipa Toba Kutisha, Frank Kahole, Nickson Kibabage, Jofrey Luseke, Vedastus Mwihambi, Juma Nyangi, Nassoro Kiziwa, Balama Mapinduzi, Onesmo Mayaya, Adam Adam na Ismail Mhesa.

Kikosi cha akiba ni Razack Shekimweli, Ladaki Chasambi, Omary Sultan, Cassian Ponela, Eliuter Mpepo, George Chota, Paschal Kitenge, Omary Seleman na Joseph Mkele.

Kipa chipukizi wa timu hiyo, Razack Shekimweli amerejea kikosini akianzia benchi baada ya kukosa katika michezo minne akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, huku Paschal Kitenge nae akirudi kikosini baada ya kumaliza adhabu kutokana na kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Simba.

Chanzo: Mwanaspoti