Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar wapaa kileleni, Dodoma mkiani

Dodoma Mtibwa Ilanfya Mtibwa Sugar wapaa kileleni, Dodoma mkiani

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakata Miwa Mtibwa Sugar wamechuma alama zote tatu mbele ya Dodoma Jiji na kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara baada ya kufikisha alama 15, alama moja mbele ya Simba SC.

Katika mchezo huo ambao umepigwa kwenye Dimba la Liti Singida, ambapo Dodoma Jiji walikuwa wenyeji, bao la Mtibwa limefungwa na Ilamfya dakika ya 60 ya mchezo.

Wakulima wa zabibu, Dodoma Jiji wanasalia mkiani mwa msimamo wa #NBCPL ikiwa na alama 5. Mtibwa Sugar imecheza mechi 9 huku Dodoma Jiji ikiwa imecheza mechi 8 mpaka sasa.

Matokeo ya NBC Premier League leo

14:00 Tz Prison 2-0 Polisi Tanzania

Jeremiah Juma (P) ⚽️

Samson Mbangula ⚽️

16:00 Dodoma jiji fc 0-1 Mtibwa Sugar

Charles Ilamfya ⚽️

19:00 Namungo fc 2-1 Kagera Sugar

Lukas Kikoti ⚽️

Mbaraka Yusuph ⚽️

Jacob Massawe ⚽️

Ligi kuendelea kesho Oktoba 26, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live