Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar waitandika Dodoma Jiji Manungu

B6C9D21C 0A21 4189 A863 58C5B40CDD5E.jpeg Mtibwa Sugar waitandika Dodoma Jiji Manungu

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.

Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 30 na Charles Ilanfya dakika ya 61, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 90 na ushei.

Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya saba, wakati Dodoma Jiji FC inabaki na pointi zake 24 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live