Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar waichapa Coastal Manungu

Mtibwa Sugar 2 1 Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakishangilia moja ya magoli mchezo wa jana

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.

Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Adam Adam dakika ya pili na Juma Nyangi dakika ya 32, wakati la Coastal Union limefungwa na Mubarak Hamza dakika ya 23.

Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 za mechi 10 nafasi ya 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live