Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar waanza na moto Ligi ya Vijana U 20

IMG 4351.jpeg Wachezaji wa Mtibwa wakishangilia

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wameanza vyema Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Kundi A jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ezekiel Eusebio mawili, Athumani Makambo, Said Salum na Said Mkopi.

Mechi nyingine ya Kundi A Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Namungo FC hapo hapo, huku mechi za Kundi C Geita Gold ikiilaza KMC 2-0 na Coastal UniĆ³n ikiichapa Singida Big Stars 1-0 hapo hapo Chamazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live