Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar waanza kuichimba mkwara Azam FC

Kifaru Mtibwa Ed.jpeg Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mtibwa Sugar imesema imedhamiria kuibuka na ushindi dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Tanzania Bara ‘ASFC’ utakaochezwa Aprili 3, Azam Complex Chamazi

Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru amesema kikosi chao kipo katika maandalizi ya mwisho ya mchezo huo, huku lengo kuu ni kuondoka na ushindi ambao utawapeleka katika Hatua ya Nusu Fainali ya ‘ASFC’.

Kifaru amesema hali za wachezaji wake ziko vizuri na kwamba wanaendelea kujiweka imara katika kambi yao ya Manungu ikiwa ni hatua za mwisho za kuelekea katika mchezo huo.

Amesema wanautaka ubingwa wa FA ili kurejea katika mashindano kama ilivyofanyika kwao mara ya mwisho 2017/2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live