Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar mdomoni mwa Simba

Simba Vs Mtibwa Manungu Mtibwa Sugar mdomoni mwa Simba

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kugawana pointi mojamoja dhidi ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa kete inayofuata kwa Simba ni dhidi ya Mtibwa Sugar.

Chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda akishirikiana na Seleman Matola mchezo wao wa kwanza kukaa benchi walishuhudia ubao ukisoma Namungo 2-2 Simba.

Timu hiyo ndani ya tatu bora haijawa na mwendo mzuri na itamkosa kiungo Clatous Chama ambaye amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumchezea faulo makusudi beki wa Yanga, Nickson Kibabage katika Kariakoo Dabi.

Ikumbukwe kwamba Mtibwa Sugar mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu kwa kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 2-1 Mtibwa Sugar.

Ni Mei 3 2024 mchezo huo na unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kuoambania pointi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live