Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar mambo magumu, wachezea kichapo Manungu

IMG 6209.jpeg Mtibwa Sugar ilikubali kichapo cha magoli 2-1

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Mtibwa Sugar wamechapwa mabao 2-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana jioni Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Danny Lyanga dakika ya 22 na Najim Magulu dakika ya 87, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Juma Nyangi dakika ya 45.

Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi sita, ingawa wanabaki nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake tano mkiani baada ya wote kucheza mechi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: