Kuna uwezekano mkubwa Mtibwa Sugar wakaingia uwanjani bila kuwa na kocha kwani makocha wake wote, wamezuiwa kusimama kwenye benchi la ufundi kutokana na kutokidhi vigezo.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), hivi karibuni walitangaza makocha wote waliosoma chini ya mwaka 2020, kusoma kozi ya maboresho (refresher course) hivyo waliofanya hivyo wameruhusiwa na ambao hawakufanya, wamezuiwa.
Makocha wote wa Mtibwa Sugar kuanzia Kocha Mkuu, Kocha Msaidizi, Kocha wa Magolikipa na Kocha wa Viungo, wote hawataruhisiwa kusimama kwenye benchi.
Mtibwa Sugar kesho Agosti 17, 2023 wanatarajia kucheza na Simba SC hivyo kama mambo yatabaki kama taarifa ya TFF iliyotolewa Aagosti 15, 2023 basi huwenda Mtibwa wakakosa kocha wa kusimama kwenye benchi lao.
Kwa upande wa Simba, Kocha Msaidizi na Kocha wa Viungo nao wamekosa vigezo kwa mujibu wa taarifa hiyo.