Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa Sugar ipo sana Ligi Kuu

Mtibwa Sugar Kikosi.png Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa jumpa wa magoli 3-2

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Mtibwa Sugar imejihakikishia kucheza Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao licha ya kufungwa na Tanzania Prisons bao 1-0, katika mchezo wa marudiano wa 'Play-Off' wa kusaka tiketi ya kubaki uliopigwa kwenye Uwanja wa Manungu Complex Morogoro.

Bao la Prisons lilifungwa na Mudathir Abdallah dakika ya 53 kwa 'Tik-taka' kali baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Mtibwa Sugar.

Kwa matokeo haya yanawafanya Mtibwa kusalia Ligi Kuu kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 3-2, baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Julai 3, kwenye Uwanja wa Sokoine kushinda 3-1.

Kwa upande wa Prisons wao bado wataendelea kucheza mchezo mwingine wa 'Play'Off kutafuta nafasi ya kubaki itakapopambana na JKT Tanzania inayoshiriki Ligi ya Championship baada ya kufanikiwa kuiondosha Kitayosce kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchujo.

JKT Tanzania itaanzia nyumbani kwenye mchezo wa kwanza utakaopigwa Julai 9, kabla ya Prisons kumalizia Sokoine katika mechi ya marudiano itakayochezwa Julai 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live