Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa: Hatoki mtu Gairo

9832f73a7e47c83019d4d706c763f7c8.png KLABU ya Mtibwa Sugar

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Mtibwa Sugar baada ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Azam FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM, Gairo Morogoro, wamesema kasi yao wataendeleza katika michezo mitatu iliyobaki.

Ushindi katika mchezo huo umeipandisha Mtibwa Sugar kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 15 hadi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 41 na kujipa matumaini ya kusalia ligi kuu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema michezo iliyobaki ni kupambana kufa au kupona kupata pointi tatu kwa kila mchezo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kuendelea kubaki kwa msimu ujao.

“Tumebakisha mechi tatu dhidi ya KMC tutacheza nao Jumamosi, dhidi ya Yanga na dhidi ya Ruvu Shooting na zote tutacheza kwenye Uwanja wa CCM Gairo, tumejipanga vizuri kuhakikisha mechi zote tunashinda,”alisema.

Kifaru alisema kwa sasa wanautazama mchezo ulioko mbele yao utakaochezwa kesho dhidi ya KMC kwani wamejipanga kuhakikisha wanashinda. Alisema wapo kwenye nafasi ambayo siyo salama sana na wapinzani wao KMC wakiwa pia, wanapambana ila hawana cha salia mtume lazima washinde.

Kifaru alisema watamkosa mchezaji Rifat Msuya hatokuwepo kutokana na kukabiliwa na majeraha aliyopata mchezo uliopita dhidi ya Azam FC.

Chanzo: habarileo.co.tz