Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtibwa, Azam vita ya alama tatu

Mtibazam Mtibwa wanaikaribisha Azam FC leo

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitawaka kweli kweli kwenye Uwanja wa Manungu leo Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni ambako kutapigwa mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Azam, ambayo inafukuzia kukaa kileleni mwa msimamo.

Sare tu inatosha kuifanya Azam yenye pointi 20 sawa na vinara Yanga, kupanda kileleni mwa msimamo, lakini kwa sababu Simba iliyo katika nafasi ya tatu kwa pointi 18 itacheza dhidi ya timu ya mkiani ya Ihefu baadaye leo saa 1:00 usiku, Wanalambalamba wanahitaji kushinda ili kujihakikisha kubaki kileleni angalau hadi kesho ambako Yanga itaivaa Kagera Sugar jijini Mwanza.

Azam ikishinda leo itaongoza msimamo wa ligi, lakini itakuwa imecheza mechi tatu zaidi ya Yanga, ambayo imecheza mechi nane hadi sasa.

Mtibwa ipo nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 10, kushinda nne, sare tatu na kupoteza tatu ikivuna alama 15 na inahitaji ushindi ili ifikishe 18 na kupanda hadi nafasi ya tano.

Kocha wa Mtibwa, Salumu Mayanga amesema: “Azam ni timu nzuri na tutaingia uwanjani kwa tahadhari licha ya kwamba tupo nyumbani na lengo ni kuhakikisha tunapata alama tatu.”

Kaimu kocha mkuu wa Azam, Kally Ongala alisema anafurahia mwenendo wa kikosi chake na anatarajia kuona soka safi kutoka kwa vijana hao wa Chamazi.

Msimu uliopita Azam ilikuwa mbabe kwa Mtibwa ikishinda mechi zote mbili, ambapo mchezo wa kwanza Nov.30, 2021 iliwalaza 1-0 na marudiano Mei, 21, mwaka jana Mtibwa ilichapwa mabao 2-1 nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live