Yanga ilicheza Mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Mlinzi wa kushoto katika Kikosi hicho Nickson Kibabage alipata nafasi ya kuanza katika mchezo huo.
Kibabage alionesha mchezo mzuri ingawa hakuwainua moja kwa moja Wananchi jukwaani lakini ni maamuzi sahihi ya Clement Kibabage ndio yaliwafanya watu wainuke kupitia bao la Kennedy Musonda.
Angeweza kufanya maamuzi tofauti na yale kwani alikuwa na option 2, kupiga shuti au kueka mpira ndani na akafanya maamuzi ya kueka mpira ndani akivunja mistari miwili ya JKT mpaka mpira kumfikia mfungaji.