Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtawala wa Qatar kutembelea Ufaransa, Mbappe aalikwa

Sheikh Tamim Bin Hamad.jpeg Mtawala wa Qatar kutembelea Ufaransa, Mbappe aalikwa

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtawala wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Thani anatakuwa na ziara ya siku mbili Nchini Ufaransa kuanzia leo Februari 27, 2024 ambapo atakutana na Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo matukio ya Gaza na mkwamo wa kisiasa nchini Lebanon.

Taarifa ya Ikulu ya Ufaransa ya Elysee imesema ziara hiyo itakuwa fursa ya kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili katika ulinzi, usalama, uwekezaji na uchumi.

Mshambuliaji wa PSG ambaye yupo ukingoni kutua Real Madrid, Kylian Mbappé ni miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla ya mapokezi ya Sheikh Tamim anayetua Nchini humo kwa mara ya kwanza tangu ashike kiti cha ufalme wa Qatar mnamo 2013.

Itakumbukwa Macron pamoja na Sheikh Tamim na Nasser al Khelaifi walikuwa sababu ya Mbappé kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia PSG miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo uwepo wa Mbappé kwenye hafla hiyo hauna maana ya kumbakisha Paris Saint German bali unalenga kuwaleta pamoja watu wa michezo, hivyo Mbappe ni uso pekee kutoka upande wa soka kualikwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live