Mshambuliaji Chipukizi Mtanzania, Omary Ally Marungu amesajiliwa na klabu ya Hapoel Kfar Saba FC ya Israel akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mchezaji huyo aliyeng'ara katika ligi ya vijana ya U20 msimu uliopita akiiwezesha Mtibwa Sugar kutwaa ubingwa amesajiliwa na klabu hiyo ya Daraja la Kwanza Israel, ijulikanayo kama Liga Leumit baada ya kufuzu majaribio aliyofanya kuanzia mapema mwezi huu.
Anakuwa Mtanzania mwingine kucheza Israel kwa sasa baada ya kiungo Novatus Dismas Miroshi, anayecheza timu Beitar Tel Aviv Bat Yam FC ya Liga Leumit pia kwa mkopo kutoka Maccabi Tel Aviv aliyojiunga nayo mwaka jana kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.