Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania asaini Mkataba Al-Hilal ya Sudan

David Richard Ulomi.jpeg Mchezaji David Ulomi anaetajwa kujiunga na Al-Hilal

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga chipukizi Mtanzania, David Richard Ulomi amejiunga na klabu ya Al-Hilal ya Sudan kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Dodoma Jiji FC.

Japokuwa klabu ya Dodoma Jiji imepinga suala hilo wakidai ni tetesi tu na Ulomi ni mchezaji wao isipokua ameomba ruhusa kwenda Dar es Salaam kwa masuala ya kifamilia.

Akizungumza mmoja wa Viongozi wa Dodoma Jiji amesema; "Hakuna taarifa yoyote rasmi ambayo imetoka kwetu wala kwa Al-Hilal inayohusu kumnunua Richard Ulomi, kwa sisi kwetu hilo jambo halipo ni fununu tu ila kama mnaweza jaribuni kuwatafuta Al-Hilal" amesisitiza kiongozi huyo

"Mchezaji bado ni mali ya Dodoma Jiji, na hivi sasa yupo nje ya kambi kwa ruhusa maalum ya uongozi, amekwenda Dar es Salaam kwa ajili ya masuala ya kifamilia"

Richard Ulomi yeye binafsi amekiri kuondoka Dodoma na kujiunga na Klabu hiyo huku akiishukuru kampuni ambayo inamsimamia.

"Dili lote hili limeratibiwa na Kampuni yangu inayonisimamia, lakini katika suala la malipo kidogo wapo vizuri kuliko kule nilikotoka ila tu napenda kuitumia nafasi hii kama ngazi ya kupanda na kuelekea kule ninapopataka" amesema Ulomi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live